Yanga SC

MTUPIAJI NAMBA MOJA WA YANGA KASEKE ATAJA ANAOWEZA KUCHEZA NAO

admin February 14, 2021 3:47 am


 MTUPIAJI namba moja ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Cedrick Kaze, Deus Kaseke amesema kuwa yeye anacheza na mchezaji yoyote ambaye atapangwa naye.

Kaseke kwenye upande wa watupiaji kwa vinara hao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 anashika namba moja akiwa ametupia jumla ya mabao matano.

Bao lake la tano aliitungua timu ya Mbeya City wakati wakitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na kugawana pointi mojamoja.

Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza ikiwa imekusanya jumla ya pointi 45 baada ya kucheza jumla ya mechi 19 huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 17 na pointi zake 15 imecheza jumla ya mechi 19.

Kaseke amesema:”Kila mchezaji ndani ya kikosi ni muhimu na ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi nami hivyo ni maamuzi ya mwalimu, ninacheza na mchezaji yoyote ambaye nitaanza naye.

“Kikubwa ambacho tunakifanya ndani ya uwanja ni kupambana kusaka matokeo na imani yetu kwamba jambo letu litatimia, mashabiki watupe sapoti,”.

NAMUNGO:YALITOKEA NI SOMO KWETU, TUNARUDI TANZANIA KUJIPANGA GURDIOLA:SINA MTU MAALUMU WA KUPIGA PENALTI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply