Yanga SC

YANGA: MASHABIKI TAMBENI,MSIWE WANYONGE

admin February 15, 2021 9:47 am

 


Anaandika Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze:- 

Mwanachama na shabiki wa Yanga, kwanini ukajikosesha amani kwa timu kutoka sare na kuaminishwa kuwa timu haitopata matokeo na wewe unaamini hilo.

Kumbuka mpaka sasa tuko kileleni (namba moja) kwenye msimamo wa ligi na pia tukiwa na rekodi sahihi ya kutopoteza mchezo hata mmoja.

Lazima tukubaliane na matokeo ya mpira na sio kulaumu sana kana kwamba tuko nafasi ya 8 au tunaburuza mkia.

Tambeni mtaani, msitembee kinyonge, vimbeni mtaani na muendelee kuipa hamasa timu yetu Insha Allah kila kitu kitaenda sawa.

Kisha tukutane Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumatano kwenye mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar saa 1:00 usiku tujitokeze kwa wingi bila kukosa.

MSIMAMO WA LIGI KUU BARA UPO NAMNA HII BIASHARA UNITED YAVUNJA UTEJA MBELE YA MWADUI FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply