Ligi Kuu

MATOKEO MABOVU YAMTISHA KOCHA MKUU WA COASTAL UNION, JUMA MGUNDA

admin February 26, 2021 3:47 pm

 


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa anatishika na mwendo ambao wanakwenda nao ndani ya Ligi Kuu Bara jambo ambalo linawafanya watulie kidogo ili kwenda sawa na kasi ya ligi.

Ikiwa ndani ya Dodoma iliyeyusha pointi sita kwa kufungwa mbele ya JKT Tanzania na Dodoma Jiji, mechi zilichezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi zake 23 baada ya kucheza jumla ya mechi 21.

Mgunda amesema kuwa anatambua matokeo ambayo wanayapata si rafiki kwao ila watapambana kupata matokeo chanya.

“Ni kweli kwa sasa tumekuwa na matokeo ambayo si mazuri jambo ambalo linanitisha lakini kwa kuwa mimi ni mwalimu haina haja ya kuogopa haya ambayo yanatokea.

“Bado kuna mechi nyingi za kucheza na imani yangu ni kwamba tutapata matokeo chanya kwenye mechi zetu hivyo kikubwa ni wachezaji kuzidi kupambana ili kupata matokeo chanya,” amesema. 

HILI HAPA JESHI RASMI LA SIMBA DHIDI YA AFRICAN LYON, KOMBE LA SHIRIKISHO KUMBE CHIDI BEENZ ALIKUWA MTU WA MIZINGA, ALIMUIBUKIA MPAKA WAZIRI WAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply