Simba SC

BAADA YA KUWAFUNGA…AL AHLY WAJIPANGA KUMNG’OA LUIS MIQUISSONE SIMBA

admin February 27, 2021 3:48 pm

 


WAARABU wamechukizwa na kipigo. Bao la kiungo mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone dhidi ya Al Ahly linaelezwa kwamba limewafanya mabosi wa klabu hiyo ya Misri kutaka kumng’oa Konde Boy.

Luis alifunga bao pekee la ushindi katika mchezo wao wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwafanya Simba waongoze kundi A ikiwa na pointi sita.

Hii inakuwa sio kwa mara ya kwanza mchezaji huyu kuhitajika na klabu mbalimbali, lakini mabosi wa Simba wamekuwa wagumu kumuachia.

Pia inaelezwa ugumu wa mkataba wake unachangia mchezaji huyo kutoondoka kwani wakati anasajilkwa akitokea Ud Songo alisaini mkataba wa miaka mitatu na nusu Msimbazi.

YANGA YATINGA 16 BORA, NGUMI YAMPONZA MUANGOLA ALIMWA KADI NYEKUNDU MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply