Home Yanga SC CARLINHOS ATAJA SABABU ZA KUTOKUCHEZA YANGA

CARLINHOS ATAJA SABABU ZA KUTOKUCHEZA YANGA


KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ amefunguka kuwa kwa sasa tayari amekwishapona majeraha yalimweka nje ya uwanja kwa muda mrefu, na kutokuonekana kwake uwanjani kunatokana na maamuzi ya benchi la ufundi na siyo majeraha.

Carlinhos aliyejiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu amekuwa akipitia kipindi kigumu cha majeraha ambayo yamemfanya kuwa nje ya uwanja tangu mwezi Novemba mwaka jana.

Nyota huyo alianza vizuri msimu huu akihusika kwenye mabao manne ya Yanga, akifunga mabao mawili na kuasisti mara mbili.

Akizungumzia maendeleo yake Carlinhos amesema: “Ni kweli hapo nyuma nilikuwa na majeraha ambayo yaliniweka nje ya uwanja kwa muda mrefu, lakini tayari nilikwishapona na kwa sasa nipo sawa kwa ajili ya kuisaidia timu yangu kupata matokeo mazuri uwanjani na kuweza kufikia malengo yetu.

“Hivyo kuhusiana na ishu ya kutokucheza, hilo ni swala lililo kwenye maamuzi ya benchi la ufundi ambayo kimsingi mimi kama mchezaji siwezi kuliongelea,”

SOMA NA HII  FT: BIASHARA UTD 1-1 YANGA ....MAYELE KAMA KAWA JAPO SIO KIVILEE...WAKIZIDI KUZINGUA SIMBA BADO YUMO UJUE...