Home Simba SC GOMES APIGA HESABU KUPUNGUZA DENI LA POINTI ZA YANGA

GOMES APIGA HESABU KUPUNGUZA DENI LA POINTI ZA YANGA


 IKIWA leo anatarajia kuiongoza timu ya Simba kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara,  Didier Gomes amesema kuwa utakuwa mchezo mgumu ndani ya dakika 90.

Leo Februari 4, Simba itakuwa ugenini kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Dodoma Jiji inayonolewa na Kocha Mkuu,Mbwana Makata.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Gomes ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kurithi mikoba ya Sven Vandenbroeck aliyebwaga manyanga Januari 7.

Michezo miwili ambayo aliongoza ilikuwa ni ile ya Simba Super Cup na alishinda mchezo mmoja dhidi ya Al Hilal mabao 4-1 na ililazimisha sare ya bila kufungana na TP Mazembe ambapo katika mchezo huo nyota wake Meddie Kagere hakucheza.

Kocha huyo amesema:”Utakuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani hasa ukizingatia kwamba kila timu inahitaji pointi tatu.  Tuna mechi tatu za kucheza nazo tunahitaji ushindi hivyo haitakuwa kazi nyepesi.

“Tuna kazi ya kupunguza pointi ambazo tumeachana na vinara wa Ligi Kuu Bara ambao ni Yanga,” .

Simba ipo nafasi ya pili na pointi 35 baada ya kucheza mechi 15 inakutana na Dodoma Jiji ambayo ipo nafasi ya 10 na pointi zake 22.

Kikosi kilitia timu jana Februari 3 Dodoma na kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa leo.

SOMA NA HII  BALEKE AANDIKA REKODI HII MOROCCO...LIGI YA MABINGWA AFRIKA