Home news HIMID MAO ATUA ENTAG EL HARBY YA MISRI

HIMID MAO ATUA ENTAG EL HARBY YA MISRI

 

KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao ‘Ninja’ amekamilisha dili la kujiunga na Entag El Harby FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri akitokea Enppi FC.

Himid amejiunga na klabu hiyo akiwa mchezaji huru, kufuatia mkataba wake na Enppi kufikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita.Himid anakuwa mchezaji wanne kusajiliwa na Entag El-Harby SC akitanguliwa na Ahmed Saber pia kutoka Enppi, Mohamed Sosta kutoka Aswan na kipa Ahmed Busca.

 Entag El-Harby SC imekuwa na mwanzo mbaya katika msimu huu, hali iliyosababisha kuburuza mkia kwenye msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na alama tano tu, baada ya kucheza michezo tisa, hivyo kusababisha kocha mkuu wa timu hiyo, Mokhtar Mokhtar kutimuliwa kazi.

 Himid Mao alianza kucheza soka Misri mnamo Julai 2018, akisajiliwa na Petrojet, lakini mwaka mmoja baadaye alihamia Enppi, akiichezea michezo 22 msimu uliopita.

SOMA NA HII  UNAIKUMBUKA ILE 'MOMENTI' YA AZIZ KI KUSHANGILIA NA MAKAMBO JUZI...BASI KUMBE NYUMA YA PAZIA KUNA HILI KATI YAO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here