Home Simba SC HUKO CONGO: SIMBA SC IMECHUKUA…IMEWEKA..WAAHHH..!!!!

HUKO CONGO: SIMBA SC IMECHUKUA…IMEWEKA..WAAHHH..!!!!


KINSHASA. WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya mabingwa Afrika Simba wamefanikiwa kukusanya alama tatu muhimu ugenini baada ya kuifunga AS Vita bao 1-0 kwenye Uwanja wa Stade de Martyrs, Kinshasa nchini DR Congo.

Simba wamefuta aibu ya kufungwa mabao 5-0 ambayo walifungwa msimu wa 2018/19 kwenye dimba hilo na sasa wameondoka kifua mbele kwa bao la penalti lililowekwa wavuni na Chris Mugalu.

Penalti hiyo imetokana na mchezaji wa AS Vita kunawa mpira uliopigwa na Luis Miquissone dakika ya 60.

Kipindi cha kwanza Simba walionekana kucheza zaidi katika nidhamu ya kuzuia kuliko kushambulia.

Muda mwingi Simba walikuwa wanacheza pasi fupi fupi katikati mwa uwanja na muda mwingine kurudisha nyuma.

Simba walifanya shambulizi moja la kushtukiza ambalo alikutana nalo, Luis Jose ingawa shuti lake ambalo alipiga lilizuiliwa na mabeki wa AS Vita.

Simba walishambulia mara chache na muda mwingi walikuwa wakijilinda kuanzia mbele ambapo alikuwa anacheza, Chriss Mugalu mwenyewe.

Mugalu ambaye alikuwa akicheza katika eneo la ushambuliaji alikuwa anaoambana na mabeki wa AS Vita akiwa mwenyewe kuna muda alifanikiwa na mpaka kuchezewa faulo ila wakati mwingine alizidiwa.

Wakati Simba wakicheza kwa kujilinda zaidi AS Vita wao walikuwa wakijitahidi kushambulia mara kwa mara ingawa hawakufanikiwa kupata bao.

Mashambulizi matatu ya hatari ambayo Vital walifanya yote yaliishia kwa mikono ya Aishi Manula ambayo mawili aliyadaka na moja alilipangua.

As Vita walifanya mashambulizi mengi kupitia kwa beki wao wa kulia, Djuma Shabani ambaye kuna muda mpaka alikuwa akichezewa faulo za mara kwa mara.

Mpaka kipindi cha kwanza Simba walifanikiwa dhumuni lao la kujilinda wakati AS Vita walishindwa kufanya vizuri kutokana walikuwa na plani za kushambulia mara kwa mara.

Kipindi cha pili Simba walianza kujiamini na kushambulia hadi kupata penalti iliyowafanya kupunguza mashambulizi na AS Vita kuanza kushambulia wakijaa langoni.

Beki wa AS Vita na nahodha wao, Djuma Shaban alikuwa mwiba kwa wachezaji wa Simba akiwasumbua Tshabalala mara kwa mara akileta madhara langoni japo hawakufanikiwa kufunga.

SOMA NA HII  MBRAZILI WA VIPERS AINGIWA NA UBARIDI NA 'VIBE' LA SIMBA KWA MKAPA...APANGA KUJA NA HILI...

Simba wamejihakikishia alama tatu na kuongoza kundi A ambalo lina timu nyingine za Al Ahly, El Merikh na AS Vita.

Mechi ya pili kwa wekundu wa Msimbazi itachezwa Februari 23 dhidi ya Al Ahly kwenye dimba la nyumbani kwa Mkapa.