Home Yanga SC KASEKE:TUTAIFUNGA KEN GOLD KESHO

KASEKE:TUTAIFUNGA KEN GOLD KESHO


 DEUS Kaseke, kiungo wa Klabu ya Yanga amesema kuwa kesho wanaamini watashinda mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Ken Gold.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni.

Kiungo huyo ambaye ametupia jumla ya mabao sita na pasi moja ya bao amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho na imani yetu ni kupata ushindi kwa kuwa inawezekana.

“Kikubwa ni suala la kusubiri na kuona itakuaje kwa kuwa wachezaji kiujumla wanahitaji ushindi na maandalizi yapo vizuri,” amesema.

SOMA NA HII  MANARA 'APIGILIA NYUNDO' ISHU YA MAYELE KUTAKIWA KAIZER CHIEF...ATUPA DONGO SIMBA...