Home Yanga SC SABABU YA FEI KUMWAGA MACHOZI BAADA YA KUGAWANA POINTI NA KAGERA SUGAR

SABABU YA FEI KUMWAGA MACHOZI BAADA YA KUGAWANA POINTI NA KAGERA SUGAR


KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum amesema kuwa machozi aliyoyatoa wakati wakigawana pointi mojamoja na Kagera Sugar yalitokana na gharama ya timu hiyo kupambana ndani ya dakika 90 na kushindwa kuambulia pointi tatu. 

Februari 17, Yanga ilikubali sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa na ulikusanya jumla ya mabao sita ndani ya Uwanja wa Mkapa ikiwa ni idadi kubwa ya mabao kukusanywa kwa mechi zote ambazo zimechezwa hapo ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21.

Inakuwa ni mechi ya pili kwa Kagera Sugar kucheza na kushuhudia jumla mabao sita wakiwa uwanjani kwa kuwa walianza na ule wa Azam FC 4-2 Kagera Sugar ila ilikuwa ni Uwanja wa Azam Complex.

Fei Toto ambaye dakika za lala salama alimtengenezea pasi mshikaji wake Ditram Nchimbi ambaye kabla hajauzamisha nyavuni, Mlipili Yusuph alitibua mipango hiyo na kuwaacha mashabiki na wachezaji wasiamini wanachokiona.

Nyota huyo amesema:”Machozi yangu yalikuwa ni maumivu ya kushindwa kupata pointi tatu licha ya timu kupambana ndani ya dakika 90.

“Kwa kile ambacho tumekipata tunaahidi kupambana zaidi kwa ajili ya mechi zetu zijazo ili tuweze kupata pointi tatu,mashabiki watupe sapoti,” .

Ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 46 kesho inakutana na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku, kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Yanga ilishinda bao 1-0, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

SOMA NA HII  GAMONDI AWAWEKEA MKAKATI WA HATARI KMC LEO