Simba SC

LUIS NA MANULA NI HABARI NYINGINE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

admin March 2, 2021 2:47 pm


 NYOTA wa Simba Luis Miquissone na kipa namba moja Aishi Manula majina yao yamekuwa yakitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji mahiri ndani ya uwanja pamoja na kutimiza majukumu yao kwa umakini.


Baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambao ulikamilika kwa Simba kushinda bao 1-0 dhidi ya Al Ahly, ukurasa wa Instagram wa Cafclcc ulimtambulisha Manula kuwa kipa aliyeokoa mchomo hatari kutoka kwa wapinzani wao Al Ahly.

Msumari huo ulipigwa dakika za lala salama baada ya beki Joash Onyango kuzidiwa ujanja na wachezaji wa Al Ahly na lilikuwa ni jaribio la kwanza lililolenga lango.

Leo Machi 2, ukursa huo ambao ni rasmi kwa ajili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika umelitambulisha bao la Luis kuwa bora.

Ni lile ambalo aliwafunga Al Ahly ilikuwa ni Februari 23 na Simba ilishinda bao hilo lililodumu kwa muda wa dakika 60 bila wapinzani wao kuweka mzani sawa.

THIAGO AAMBIWA KWAMBA ALIPASWA KUCHEZA MANCHESTER UNITED ALIYEWATUNGUA YANGA HAT TRICK AOMBA NAMBA KWA KAZE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply