Azam FC

AZAM WATAMBA KUMALIZA UTEJA LEO

admin March 3, 2021 9:47 am


NAHODHA wa kikosi cha klabu ya Azam, Aggrey Morris amefunguka kuwa kikosi hiko kimejipanga vizuri kuhakikisha wanamaliza uteja wa kupata matokeo katika uwanja wa Kaitaba kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Kagera Sugar, inayonolewa na kocha, Mecky Maxime.

Azam Jumamosi iliyopita iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbuni katika mchezo wa kombe la FA na kutinga hatua ya 16 bora, ambapo wamekiri kuwa ushindi huo umeongeza morali ya kupambana kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Kagera Sugar.

Azam inakamatia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa tayari imecheza michezo 21, na kujikusanyia pointi 37.

Akizungumzia mchezo huo, Morris alisema: “Kwanza tunajua wazi kuwa tunakwenda kucheza mchezo mgumu dhidi ya Kagera Sugar, mara zote tumekuwa na wakati mgumu kupata ushindi kwenye uwanja wa Kaitaba.

“Lakini wakati huu tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunaibuka na pointi tatu muhimu dhidi yao, na tutapambana kutekeleza maagizo ya benchi la ufundi ili kuhakikisha tunalifanikisha hilo,”

YACOUBA, JEMBE LA KAZI NDANI YA YANGA KUIBUKIA MKWAKWANI BAADA YA KUONGEZA MKATABA, KANGWA KUANZA NA POINTI ZA KAGERA SUGAR

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply