Simba SC

BOCCO ATOA KAULI YA KISHUJAA SIMBA AKIPAA SUDANI LEO

admin March 3, 2021 4:37 am


NAHODHA wa klabu ya Simba, John Bocco amesema mchezo wao dhidi ya Al Merreikh utakuwa mgumu lakini watahakikisha wanapambana ili kupata matokeo mazuri.

“Ni mechi ya kimataifa naamini tutajipanga vizuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri dhidi yao”.

Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Sudan kwa ajili ya mchezo wao wa hatua ya makundi utakaopigwa Jumamosi Machi 6 saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Simba inaongoza kundi A ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi zake mbili dhidi ya As Vita ugenini 1-0 na Al Ahly wakiwa nyumbani 1-0.

GSM WAFUNGUKA KUHUSU TAARIFA ZA KAZE KUFUKUZWA YANGA KENEDY JUMA:ILIKUWA NDOTO YANGU KUCHEZA MASHINDANO YA KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply