Simba SC

GOMES :- TULIENI…HAWA EL MERREIKH NAWAJUA NNJE NDANI

admin March 3, 2021 5:27 am


Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema kuwa watanzania na mashabiki wa soka nchini, hususani wa Simba SC watulie wale biriani wakati huu ambapo kikosi chake kinaenda nchini Sudani kucheza mechi dhidi ya El Merreikh siku ya Jumamosi ya 6/3/2021.

Gomes amesema kuwa wamejindaa vyema ili kupata matokeo nchini Sudani, huku akiweka wazi kuwa lengo lao ni kuibuka na ushindi utakaowawezesha kufuzu mapema kwenda hatua ya Robo Finali ya michunao ya Klabu Bingwa Afrika 2020/21.

Kocha huyo Mfaransa ameongeza kuwa uozefu alionao nchini Sudani na kuwajua vyema El Merreikh ni silaha kubwa inayompa uhakika wa kujiamini kuibuka na ushindi siku hiyo.

Gomes ambaye ameiongoza Simba katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa walizoshinda kibabe ugenini dhidi ya AS Vita na nyumbani dhidi ya mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri, amesema mechi itakuwa ngumu lakini ushindi ndio lengo namba moja.

“Tunakwenda kucheza na timu ambayo naifahamu vizuri, tumeandaa mbinu nyingi za kwenda kukabiliana nao ili kuhakikisha tunapata pointi nyingine ugenini ingawa tunatambua si jambo rahisi,” alisema na kuongeza:

“Tumefanya maandalizi ya kutosha kulingana na ambavyo tumewaona wapinzani wetu. Tutatumia udhaifu wao kuwazidi ili kufanya vizuri na ninaamini itakuwa hivyo.

“Wamepoteza mechi mbili, moja nyumbani kwao na nyingine ugenini, hili litaongeza ugumu wa mechi yetu, watataka kupata ushindi wa kwanza, tupo tayari kwa hilo na tutapambana nao,” alisema kocha huyo Mfaransa.

 

MO DEWJI AWAWEKEA WACHEZAJI WA SIMBA SC MILIONI 200 MEZANI ZA KUIUA EL MERREIKH KWAO WATANO WA YANGA KUIKOSA COASTAL UNION MKWAKWANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply