MZUNGUKO WA PILI MAMBO YALIKUWA MAGUMU KWA KAZE, CHEKI REKODI ZAKE
MZUNGUKO wa pili, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze mambo yalikuwa magumu kwake kutokana na kushindwa kupata matokeo chanya kwenye mechi zake 6 za Ligi Kuu Bara aliweza kushinda mechi moja.
Ndani ya dakika 540 alipokuwa akisaka pointi 18 aliambulia jumla ya pointi 7 na kuangusha pointi 11.
Alishinda mchezo mmoja, alipoteza mchezo mmoja na kukusanya jumla ya sare nne ambazo zilimpa pointi nne na kumfanya jumla awe na pointi 7 ndani ya uwanja katika mechi 6.
Alianza sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, Mbeya City 1-1 Yanga, Yanga 3-3 Kagera Sugar na alishinda mbele ya Mtibwa Sugar bao 1-0.
Kichapo ilikuwa mbele ya Coastal Union kwa kichapo cha mabao 2-1 na mchezo wake wa mwisho ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania kwenye sare ya kufungana bao 1-1, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Jana Machi 7, yeye pamoja na benchi lake la ufundi wamefutwa kazi jumlajumla.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.