Simba SC

GOMES: TUNA SAFU BORA YA ULINZI

admin March 13, 2021 12:47 pm


KOCHA mkuu wa kikosi cha klabu ya Simba, raia wa Ufaransa, Didier Gomes amesema kuwa anafurahia kuona safu ya ulinzi ya kikosi chake ikionyesha kuimarika katika siku za hivi karibuni.

Gomes mpaka sasa hajaonja machungu ya kupoteza mchezo ndani ya kikosi cha Simba, ambapo tayari ameiongoza timu hiyo kwenye michezo tisa ya mashindano rasmi, akishinda mara sita na kutoa sare tatu.

Akizungumzia ubora wa kikosi chake Gomes amesema: “Nafurahi kuona kikosi changu kikiwa imeimarika sana katika siku za karibuni kulinganisha na hapo awali, tunaonekana kuwa na ubora mkubwa katika kuzuia kwa kuwa tumefanikiwa kupunguza idadi ya mabao ya kufungwa,”

Simba kesho kutwa Jumanne inatarajiwa kucheza mchezo wao wa nne wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Merrikh, utakaopigwa siku ya Jumanne ya wiki ijayo.

HIMID MAO AJIUNGA NA STARS KUTOKEA MISRI MSERBIA HUYU AZUNGUMZA NA YANGA KUJA KUBEBA MIKOBA YA KAZE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply