Taifa Stars

HIMID MAO AJIUNGA NA STARS KUTOKEA MISRI

admin March 13, 2021 12:47 pm


KIUNGO mkabaji wa Tanzania, Himid Mao anayecheza soka la kulipwa katika kikosi cha klabu ya Entag El Harby ya Misri tayari amejiunga na kikosi cha Taifa Stars, kwa ajili ya michezo miwili ya kujipima nguvu dhidi timu ya Taifa ya Kenya.

Michezo hiyo ambayo inatarajiwa kupigwa Machi 15, na 18 mwaka huu ni sehenu ya maandalizi ya michezo ya kusaka tiketi ya michezo ya kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), dhidi ya Equatorial Guinea na Libya.

Stars inatarajia kucheza na Equatorial Guinea Machi 25, na kukutana na Libya Machi 28, au 30 kuendana na ratiba ya Shirikisho la soka Afrika (Caf).

Nado alikuwa kwenye kikosi cha Stars kilichofanya mazoezi asubuhi ya leo.

MWL KASHASHA : MICHAEL SARPONG BADO SANA, ANAKIMBIAKIMBIA UWANJANI TU GOMES: TUNA SAFU BORA YA ULINZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply