BEKI kisiki wa Klabu ya Simba, Joash Onyango amesema kuwa yupo vizuri baada ya kupata maumivu Kwenye mchezo wao dhidi ya Al Merrikh.
Jana Machi 16 wakati ubao ukisoma Simba 3-0 Al Merrikh, Onyango alipata maumivu dakika ya 43 na nafasi yake ikichukuliwa na Erasto Nyoni.
Hali yake ilionekana kuwatisha mashabiki kwa kuwa alitolewa akiwa amebebwa Kwenye machela.
Onyango amesema:”Nipo salama na ninaendelea vizuri natarajia kuelekea Kenya kwa timu ya Taifa,”