MOHAMED Hussein, ’Zimbwe’ nahodha msaidizi wa Klabu ya Simba bao lake mbele ya Al Merrikh limeweka rekodi Afrika kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kufunga katika hatua ya makundi ndani ya kikosi hicho.
Chini ya Didier Gomes, Simba inayoongoza kundi A na pointi 10, imefunga jumla ya mabao matano manne yote yalifungwa na wageni hivyo bao lake limeweka rekodi kwa msimu wa 2020/21.
Mabao hayo ya Simba yalifungwa na Chris Mugalu mwenye mabao mawili, mbele ya AS Vita na Al Merrikh yeye ni raia wa Congo, Luis Miquissone ana mabao mawili alifunga mbele ya Al Ahly na Al Merrikh.
Bao la kwanza la mzawa ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Simba limefungwa na Zimbwe, Uwanja wa Mkapa yeye ni beki wa kushoto chaguo namba moja la Gomes.
Pia jina limetajwa kwenye orodha ya kikosi bora cha wiki ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mechi nne hivyo anakuwa mzawa wa kwanza kuingia kwenye kikosi.