Simba SC

GOMES AMPA TANO MSHAMBULIAJI WAKE CRIS MUGALU

admin March 20, 2021 1:47 pm


KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Mfaransa Didier Gomes amefunguka kwamba anakoshwa sana na straika wake, Mkongomani Chris Mugalu kutokana na namna ambavyo amekuwa akibaki kwenye hali ya kujiamini hata anapofanya vibaya.

 

Gomes ameongeza kwamba straika huyo anaifanya kazi yake vizuri katika mfumo ambao amekuwa akiutumia wa mshambuliaji mmoja ambapo amekuwa na hali ya kujiamini kwa kiwango kikubwa mbele ya wapinzani wao.


Katika mfumo wa kocha huyo wa Simba 4-2-3-1, Mugalu ndiye amekuwa akitumika kama mshambuliaji halisi wa kati akiwa anacheza peke yake.

 

Gomes amesema kuwa straika huyo amekuwa akifanya katika eneo hilo ambalo anampanga kwa kuwa amekuwa akijiamini mbele ya mabeki wa timu pinzani kitu ambacho ni faida kwao.


β€œKwenye mfumo huu wangu, straika mmoja anahitaji kujiamini zaidi, hilo ni muhimu na nimeliona kwa Mugalu. Amekuwa akifanya hivyo na anafunga mabao ikiwemo mechi yetu iliyopita na Merrikh.

 

β€œNi kitu kizuri kwake kujiamini, kwa sababu inakuwa faida kwetu. Lakini hata wenzake Meddie (Kagere) anafanya vizuri na nahodha wetu John (Bocco) naye amekuwa akifanya hivyo pale ambapo anacheza. Najivunia naye.

TIMU ZA BONGO ZIMEACHIWA DENI LA KULIPA NA MAGUFULI NAMUNGO KUANZA KUIWINDA NKANA KESHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply