Namungo FC

NAMUNGO KUANZA KUIWINDA NKANA KESHO

admin March 20, 2021 2:47 pm


KIKOSI cha klabu ya soka ya Namungo kesho Jumapili kinatarajia kuanza rasmi mazoezi ya kujiwinda na mchezo wao wa tatu wa makundi kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Ijumaa ya Aprili 2.

Namungo inakamatia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi D la michuano hiyo ikiwa bado haijapata alama yoyote.

Pyramids na Raja Casablanca ndiyo vinara wa msimamo na pointi zao sita, huku Nkana wao wakiwa wanabuluza mkia baada ya kufungwa michezo yao miwili kwa idadi kubwa ya mabao kulinganisha na Namungo.

Akizungumzia mipango yao, Ofisa habari wa klabu ya Namungo Kindamba Namlia amesema: “Kikosi chetu kinatarajia kuanza rasmi mazoezi kesho Jumapili, kwa ajili ya mchezo wetu ujao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Nkana utakaochezwa Aprili 2, mwaka huu,”

GOMES AMPA TANO MSHAMBULIAJI WAKE CRIS MUGALU YANGA: MAGUFULI ALIKUWA NA BAHATI NA SISI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply