KIUNGO YANGA AIFAGILIA SIMBA
Kiungo wa zamani wa Yanga, Zawadi Mauya kiwango kinachoonyeshwa na mastaa wa Simba ndiyo chachu ya mafanikio yao msimu huu.
Nyota wa Simba waliosajiliwa dirisha dogo na kuwa na mchango mkubwa ni viungo Libasse Gueye mwenye mabao saba, Anicet Oura mwenye mabao manne, kurejea kwa Clatous Chama mabao aliyefunga mabao manane.
“Msimu huu Simba ina ‘chalenji’ nzuri mbio za ubingwa, tofauti na misimu iliyopita ilikuwa inafungwa kirahisi na watani wao Yanga ila kwa sasa zikikutana kwenye mechi inakuwa ngumu kuanzia dakika ya kwanza hadi ya 90,” alisema Mauya na kuongeza;
“Msimu huu Simba imefanikiwa kunyakua taji la Muungano kwa kuifunga Yanga bao 1-0, imepitia milima na mabonde haijalishi msimu huu inaweza ikachukua taji la ligi au la lakini tayari imeanza kurejea katika mstari wa ushindani mkubwa.”
Alisema ikitokea Yanga ikateleza mechi hata moja, basi anaona yanaweza yakajirudia ya msimu uliyopita timu hiyo ilichukua ubingwa mechi ya mwisho kwa mabao 2-0 dhidi ya Simba iliyopigwa Juni 25,2025, huku klabu hizo zilitofautiana kwa pointi nne, Wanajangwani walimaliza kwa alama 82 na Simba pointi 78.