UONGOZI wa Klabu ya Njombe Mji inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza umeweka wazi kuwa kuondoka kwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ni pigo kwa taifa na dunia kiujumla.
Akizungumza Championi Jumamosi, Saleh Nyenzi, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji alisema kuwa kutokana na msiba huo hawataweza kucheza mechi ya aina yoyote huku wakiendelea kumuombea kiongozi huyo.
βKwa kweli ni pigo kwa taifa na kwa sasa ni huzuni ambayo imetawala kwani alikuwa ni moja ya viongozi wa mfano katika kutimiza majukumu yake na alikuwa ni mpenda michezo.
βKwa wakati huu timu bado ipo kambini nasi pia tunamuombea Magufuli apumzike kwa amani, tunawaomba Watanzania wazidi kumuezi kwa mema aliyofanya,β alisema.