news

NJOMBE MJI WAMLILIA JOHN MAGUFULI

admin March 20, 2021 10:47 am

 


UONGOZI wa Klabu ya Njombe Mji inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza umeweka wazi kuwa kuondoka kwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ni pigo kwa taifa na dunia kiujumla.

Akizungumza Championi Jumamosi, Saleh Nyenzi, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji alisema kuwa kutokana na msiba huo hawataweza kucheza mechi ya aina yoyote huku wakiendelea kumuombea kiongozi huyo.

“Kwa kweli ni pigo kwa taifa na  kwa sasa ni huzuni ambayo imetawala kwani alikuwa ni moja ya viongozi wa mfano katika kutimiza majukumu yake na alikuwa ni mpenda michezo.

“Kwa wakati huu timu bado ipo kambini nasi pia tunamuombea Magufuli apumzike kwa amani, tunawaomba Watanzania wazidi kumuezi kwa mema aliyofanya,” alisema.

SIMBA YAPANIA KUTIMIZA AHADI YA MAGUFULI KWA VITENDO MO DEWJI AWEKA MILIONI 500 MEZANI KUIFUNGA AS VITA DAR

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply