Simba SC

SIMBA WAJIPANGA KUIMALIZA AS VITA

admin March 20, 2021 3:47 pm


KIKOSI cha wachezaji wa klabu ya Simba ambao hawajaitwa kwenye vikosi vya timu zao za Taifa, tayari wameanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita.

Simba na AS Vita zinatarajia kukutana Jumamosi ya Aprili 3, katika mchezo wa tano wa kundi A la michuano hiyo, ambapo mpaka sasa Simba ndiyo kinara wa kundi hilo baada ya kujikusanyia pointi 10.

Akizungumzia kuhusu maandalizi hayo, Meneja wa kikosi cha klabu ya Simba, Patrick Rweyemamu amesema: “Kikosi cha wachezaji wetu ambao hawajaitwa kwenye timu za Taifa wameanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu wa tano wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya DR Congo Jumamosi ya Aprili 3, mwaka huu.

“Kuelekea mchezo huo, sehemu ya nyota wetu ambao hawajaitwa kwenye vikosi vya timu za taifa tayari wameanza mazoezi kwa ajili ya mchezo huo,”

YANGA: MAGUFULI ALIKUWA NA BAHATI NA SISI KONDE BOY, ZIMBWE JR WA SIMBA WATAJWA KIKOSI BORA AFRIKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply