UONGOZI wa Yanga umewaomba mashabiki wasiwe na presha juu ya mwendo wao ndani ya ligi kwa kuwa wanaamini kwamba watarejea kwenye ubora.
Machi 7, Yanga walimfuta kazi Cedric Kaze raia wa Burundi na msaidizi wake Nizar Khalfan ambaye ni mzawa kwa kile ambacho walieleza kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo.
Kwenye mzunguko wa pili kwenye mechi sita, Kaze aliongoza kikosi hicho kushinda mechi moja, sare nne na alipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union.
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa yote ambayo wanapita ni kipindi cha mpito yatakwisha na maisha yataendelea.
“Tukiwa ni timu tunatambua kwamba mashabiki wanahitaji kuona tunapata matokeo hilo ni jambo jema nasi tunalifikiria. Kuyumba ni kwa muda tunaamini kwamba tutarejea kwenye ubora na kila kitu kitakwenda sawa.
“Ikiwa shabiki utasema ukate tamaa wakati huu bado ni mapema na ligi haijakamilika, hivyo muhimu ni kubaki kwenye malengo yetu na kuzidi kupambana,” .