SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa zamani wa Klabu ya Simba amesema kuwa kuondoka kwa Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli ni pigo kwa Tanzania na dunia jambo ambalo anatoa pole.
Vandenbroeck raia wa Ubelgiji alikuwa ndani ya Simba zama za utawala wa Magufuli na alishuhudia namna maendeleo ya soka yalivyokuwa yakipambaniwa na watendaji kazi wa Magufuli.
Kwa sasa yupo zake nchini Morocco akiendelea na majukumu yake baada ya kubwaga manyanga ndani ya Simba , Januari, 2021.
Kocha huyo amesema:”Pole Tanzania ni machozi kwetu pia kwa kuondoka kwake, pole Tanzania, pumzika kwa amani Magufuli,” .
Vandenbroeck alihudumu Simba kwa msimu mmoja ambapo alitwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 baada ya kumaliza kazi iliyoanzishwa na Patrick Aussems, aliipa pia Kombe la Shirikisho pamoja na ngao ya jamii.
Pa aliipeleka Simba hatua ya makundi na mchezo wake wa mwisho alishinda mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum Uwanja wa Mkapa.