Taifa Stars

MBWANA SAMATTA ANAAMINI KWAMBA STARS WATAFANYA VIZURI KESHO

admin March 24, 2021 6:47 am


MBWANA Samatta, nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Equatorial Guinea ambao ni maalumu kwa ajili ya kusaka tiketi ya kufuzu AFCON.

Stars chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen iliweka kambi nchini Kenya ambapo ilicheza mchezo wa kirafiki mmoja dhidi ya Kenya na ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Samatta amesema:”Tunatambua kwamba tuna kazi kubwa ya kufanya kusaka ushindi kwenye mchezo wetu dhidi ya Equatorial Guinea hilo lipo wazi.

“Ukweli ni kwamba mwalimu ambaye tupo naye anatutambua vizuri kwa kuwa nilifanya naye kazi kwenye timu za vijana na sasa tupo naye kwenye hii timu kubwa ni furaha kwetu.

“Mashabiki wazidi kutuombea dua ili tufanye vizuri nasi tutapambana ili kupata matokeo chanya kila kitu kinawezekana,” amesema.

BUSHOKE: MAGUFULI ALIKUWA MTETEZI WA WANYONGE MCHAKATO WA KUMSAKA KOCHA MPYA YANGA UMEFIKA HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply