Yanga SC

MCHAKATO WA KUMSAKA KOCHA MPYA YANGA UMEFIKA HAPA

admin March 24, 2021 6:47 am




UONGOZI wa Yanga umesema kuwa licha ya kwamba timu ipo mikononi mwa Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi hawatasimamisha zoezi la kumsaka kocha mpya.


Yanga ilimfuta kazi Cedric Kaze, Machi 7 kwa kile ambacho walieleza kuwa matokeo yalikuwa mabovu jambo ambalo walikuwa wanatafuta kutibu tatizo hilo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominic Albinius amesema kuwa bado mchakato wa kumsaka kocha mpya unaendelea ili waweze kumpata mrithi sahihi wa mikoba ya Kaze.

“Mchakato wa kumsaka kocha mpya unaendelea licha ya kwamba kwa sasa timu ipo chini ya Mwambusi ambaye anaendelea kuisimamia timu.

“Kocha ambaye atapatikana anahitaji muda wa kuisoma timu ili atakapoanza kazi basi asipate tabu katika kusimamia majukumu yake hivyo mashabiki wasiwe na presha,” amesema.
Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 23. Kaze aliongoza timu hiyo kwenye jumla ya mechi 18 kwa kuwa tano ziliongozwa na Zlatko Krmpotic ambaye naye alifutwa kazi.

MBWANA SAMATTA ANAAMINI KWAMBA STARS WATAFANYA VIZURI KESHO SIMBA YAVUNJA REKODI YAKE ILIYOWEKA KWENYE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply