IMEELEZWA kuwa jina la Sebastian Migne lina asilimia kubwa kupitishwa kuwa kocha mkuu ndani ya kikosi hicho ambacho kinaongoza ligi kwa sasa na pointi 50.
Kamati ya Ufundi ya Yanga iliyo chini ya Dominic Albinius, itakutana Jumamosi hii tayari kwa ajili ya kumuandalia tiketi kocha huyo atakayepitishwa.
Mpaka sasa, kocha anayetajwa zaidi ni Migne aliyewahi kuzifundisha timu za taifa za Kenya, DR Congo na Guinea Ikweta.
Pia kocha mwingine ambaye anapewa nafasi ya kuja kuchukua mikoba ya Cedric Kaze ni Mserbia, Nikola Kavazovic.
Kaze alifutwa kazi Machi 7 kwa kile ambacho kilielezwa kuwa ni matokeo mabovu ya timu hiyo kwa mzunguko wa pili.
Katika mechi 6, timu ilishinda mchezo mmoja na kulazimisha sare nne huku ikipoteza kwa mara ya kwanza mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwai Tanga, ubao ulisoma Coastal Union 2-1 Yanga.