Ligi Kuu

KOCHA MPYA KAGERA SUGAR NA MATUMAINI YA KUFANYA VIZURI NDANI YA LIGI

admin March 27, 2021 7:47 am


 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Klabu ya Kagera Sugar amesema kuwa anaamini kuwa vijana wake watafanya vizuri kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mashindano mengine.

Kocha huyo aliibuka ndani ya Kagera Sugar akitokea Klabu ya Biashara United ya Mara akichukua mikoba ya Mecky Maxime ambaye alifutwa kazi kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo mbovu wa Kagera Sugar kwenye ligi.

Akiwa ndani ya Biashara United timu yake ilikuwa nafasi ya 4 na imekusanya jumla ya pointi 39 anakutana na Klabu ya Kagera Sugar ambayo ipo nafasi ya 13 na  pointi zake ni 25.

Baraza amesema:”Kazi inaanza na kwa namna ambavyo nimewaona vijana imani yangu ni kwamba tutafanya vizuri na tutarejea kwenye ubora.

“Kikubwa ni kwa wachezaji kufuata maelekezo na kufanya yale ambayo tunakubaliana kwani ushindani kwenye ligi ni mkubwa na kila mchezaji na timu kiujumla inahitaji matokeo chanya,” amesema.

Kwa sasa Klabu ya Biashara United ipo mikononi mwa Marwa Chamberi Marwa.

KIPA NAMBA MOJA WA SIMBA MANULA AFUATWA NA WAARABU BEACH SOCCER YARAHISISHIWA KAZI KUFUZU AFCON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply