Home Yanga SC KAMPUNI 10 ZA KIMATAIFA ZAJITOKEZA KUUJENGA UWANJA WA YANGA KIGAMBONI

KAMPUNI 10 ZA KIMATAIFA ZAJITOKEZA KUUJENGA UWANJA WA YANGA KIGAMBONI


MAKAMPUNI 10 ya ujenzi yamejitosa Yanga kupata nafasi ya kujenga Uwanja wa Klabu hiyo ulioko Kigamboni Dar es Salaam.

Mwishoni mwa mwaka jana, Yanga kupitia kwa Kamati ya Ujenzi na Miundombinu ilitangaza zabuni ya ujenzi wa hosteli na uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema jana kuwa wazabuni 10 wamejitosa kuomba kazi hiyo toka walipotangaza.

Mfikirwa alisema, makampuni hayo mengi ni ya Tanzania huku mengine yakiwa ya nje ya Nchi lakini yanafanya kazi zake hapa Nchini.

“Tuliweka wazi ili makampuni yanayoona yanaweza kufanya kazi hiyo yajitokeze lakini mpaka sasa ni makampuni 10 yaliyoonyesha nia hiyo.

“Tutamtangaza wazi ambaye atakuwa amepata hiyo tenda tayari kwa kuanza majukumu hayo,”alisema Mfikirwa.

Yanga kwa sasa inaweka kambi Kigamboni lakini ikifanikiwa kukamilisha ujenzi huo itakuwa imepunguza gharama kubwa za kukodi sehemu malazi.

Ikumbukwe hata watani zao Simba walijikomboa na matumizi hayo makubwa ya pesa za kukodi viwanja na kuamua kujenga uwanja wao wa mazoezi wa Mo Bunju Arena ambao umewafanya kuokoa sh 500,000 kwa siku ambazo zilikuwa gharama za kulipia viwanja.

SOMA NA HII  OKWA: YANGA WAKITOBOA KESHO KUTWA ..MJE NIMEKAA PALEE...