Home news AS VITA, TP MAZEMBE WAMLILIA RAIS MAGUFULI

AS VITA, TP MAZEMBE WAMLILIA RAIS MAGUFULI


BAADA ya kusikia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania John Magufuli, kiungo wa kati wa Klabu ya AS Vita, Jeremy Mumbere amemlilia rais huyo huku akisema kuwa yeye alikuwa ni kati ya shabiki mkubwa wa kiongozi huyo.

Jeremy Mumbere kwa sasa ni nahodha wa kikosi cha AS Vita na timu ya Taifa ya DR Congo.

Akizungumza na Championi Ijumaa moja kwa moja kutoka nchini DR Congo, Mumbere alisema kuwa amesikitishwa kusikia taarifa za kifo cha Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kwani alikuwa ni kiongozi mzuri ambaye alikuwa akimfuatilia kwa ukaribu kutokana na utendaji wake kuwa mzuri jambo ambalo lilimfanya awe anamfuatilia mara kwa mara.

“Nimesikitika sana kusikia taarifa za msiba wa Rais wa Tanzania, John Magufuli ni moja kati ya rais bora kuwahi kutokea katika bara hili la Afrika, alikuwa ni kiongozi anayependa maendeleo na Tanzania ilikuwa imepata mengi mazuri kutoka kwake.

“Utendaji wake wa kazi ulinifanya niwe shabiki yake kwa kumfuatilia kwa mambo mengi, hakika Tanzania imempoteza mtu wa muhimu sana kwani hata huku DRC tulikuwa tunampenda sana Rais Magufuli,” alisema kiungo huyo.

Naye mwenyekiti wa mashabiki wa Klabu ya TP Mazembe, Jean Mazembe Kazadi alisema: “Niwape pole Watanzania wote na Afrika kwa jumla kwa kumpoteza Rais Magufuli, nasema Afrika kwa jumla kwa kuwa ndiye alikuwa kioo kwa viongozi wengi hapa Afrika katika maamuzi ambayo wengi walikuwa hawezi kasoro yeye ambaye alikuwa akithubutu, wote tumuombee Magufuli,” alisema kiongozi huyo.

SOMA NA HII  SKUDU NA SIMBA MPAKA KIELEWEKE