Home CAF AS VITA YATUMA UJUMBE HUU SIMBA, YAPANIA KUREKEBISHA MAKOSA

AS VITA YATUMA UJUMBE HUU SIMBA, YAPANIA KUREKEBISHA MAKOSA


 KOCHA Mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge amesema kuwa ili waweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wanatakiwa kuibuka na ushindi katika michezo yao miwili iliyosalia ya ligi hiyo, dhidi Simba na Al Merrikh.

 

AS Vita kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika mara baada ya kujikusanyia pointi 4 nyuma ya Simba wenye 10 na Al Ahly wana saba.


 Kocha Ibenge amesema kuwa kulingana na matokeo na pointi ambazo wamezipata wanatakiwa kushinda michezo yao miwili ijayo bila kujali wanakutana na timu ipi kwani wasipofanya hivyo hawatakuwa na uwezo wa kusonga mbele kuelekea katika hatua ya robo fainali.

 

“Tunatakiwa kushinda michezo yetu yote miwili iliyosalia dhidi ya Simba na Al Merrikh ili tuweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali, matokeo tuliyopata hayakuwa mazuri sana kwetu lakini huu si muda wa kulaumiana tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha tunasonga mbele.

 

“Tunatakiwa kutojali tunacheza na mpinzani wa aina gani, michezo yote iliyosalia ni migumu kwetu tunacheza na Simba tukiwa ugenini mara ya mwisho tulipoteza mchezo pale hivyo hatutakiwa kurudia makosa, mchezo wa mwisho tutakuwa nyumbani kila mtu anafahamu hatujashinda hata mchezo mmoja kwetu pia tunatakiwa kurekebisha hili,” amesema kocha Ibenge.

 

AS Vita wanatarajia kucheza na Simba ugenini Aprili 3, katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar huku mchezo wa mwisho ukitarajiwa kufanyika DR Congo Aprili 9 dhidi ya Al Merrikh.


SOMA NA HII  KIPIGO CHA YANGA DHIDI YA SIMBA CHAMUIBUA MAYELE...... AFUNGUKA HAYA