Home CAF KONDE BOY, ZIMBWE JR WA SIMBA WATAJWA KIKOSI BORA AFRIKA

KONDE BOY, ZIMBWE JR WA SIMBA WATAJWA KIKOSI BORA AFRIKA


NYOTA wawili wa klabu ya Simba, Luis Miquissone na Mohammed Hussein ‘Zimbwe’, wametajwa katika kikosi bora cha wiki cha michuano ya klabu bingwa Afrika ambacho kina wachezaji 16 kutoka klabu sita.

Jumanne wiki hii Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al Merrikh ya Sudani ambapo, Luis na Zimbwe walihusika kwa kiasi kikubwa katika ushindi huo.

Luis alifunga bao moja na kuasisti bao la, Chris Mugalu huku Zimbwe yeye akifanikiwa kufunga bao moja.

Ushindi huo umeifanya Simba sasa kufikisha pointi 10 na kuongoza msimamo wa kundi A la michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

SOMA NA HII  UTAFURUKUTA WEEE...LAKINI ZIKIFIKA DK HIZI...SAKHO LAZIMA AKUTUNGUE AISEE...