Home Yanga SC MAPINDUZI KUANZA MAZOEZI YANGA

MAPINDUZI KUANZA MAZOEZI YANGA


KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Balama Mapinduzi anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi hivi karibuni, baada ya kupona jeraha lake la enka alilolipata mwezi juni mwaka jana.

Februari 24, mwaka huu Mapinduzi alimaliza muda wa wiki tano ambazo alipewa na Madaktari waliokuwa wakimhudumia nchini Afrika kusini, hivyo kumpa ruhusa ya kuanza mazoezi mepesi kabla ya kujiunga na wenzake.

Balama alipata jeraha hilo katika mazoezi ya kikosi cha Yanga kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda mwezi Juni mwaka jana, na kufanyiwa upasuaji mara mbili hivyo kuwa nje ya uwanja kwa miezi nane.

Akizungumzia hali ya nyota huyo, Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Haji Mfikirwa amesema, kuwa nyota huyo anaendelea vizuri na ataanza mazoezi mwanzoni mwa mwezi huu kwa kushirikiana na timu ya madaktari wa klabu hiyo.

“Habari nzuri kwa mashabiki, wadau na wapenzi wa klabu yetu ni kuwa kiungo mshambuliaji wetu Balama Mapinduzi anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini.

“Ambapo tunatarajia mwanzoni mwa mwezi huu ataanza programu za mazoezi mepesi kwa kushirikiana na timu ya madaktari wetu, tayari kwa ajili ya kurejea uwanjani,” alisema Mfikirwa.

SOMA NA HII  GAMONDI AWEKA WAZI MPANGO HUU KIMATAIFA YANGA