Simba SC

SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA UTATA WA KAULI YA MO NA SportPesa

admin April 1, 2021 4:47 am


 MJUMBE wa bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Klabu ya Simba, Mulami Ng’ambi amefafanua ujumbe wa mkurugenzi wake wa bodi, Mohammed Dewji baada ya kutwit na kueleza hisia zake juu ya uwekezaji wa mkataba mpya wa Klabu ya Manchester United na kuhusisha Simba na mkataba wa SportPesa.


MO aliandika:- “Man Utd italipwa kiasi cha pauni milioni 305 ambazo ni sawa na Shilingi Bilioni 700 za kitanzania kwa miaka mitano kutoka kwa (Team Viewer). Simba ya Tanzania haipati hata asilimia moja ya hiyo pesa kutoka kwa wadhamini SportPesa (Asilimia moja ya hiyo pesa ni kiasi cha Bilioni 7 za kitanzania).”

 

 

Mulami amesema:-”Watu hawakumuelewa Mo Dewji. Alichokimaanisha Mohamed Dewji alikuwa anamaanisha kwamba, hela ambayo ipo au inawekezwa kwenye mpira kama udhamini bado ni kidogo sana kulinganisha na nchi nyingine ambazo zinapata udhamini.

 

 

”Nafikiri alisema Simba haipati asilimia moja ya udhamini ambayo Manchester United wanaipata katika mkataba mpya ambao wameisaini hivi karibuni. Manayake ni kwamba ilikuwa ni kuhamasisha makampuni juu ya umuhimu wa kuongeza fedha zao kwenye mpira.

 

 

“Hakuwa akimaanisha ni SportPesa peke yake, ikumbukwe kulikuwa na makampuni mengi ambayo yalijiondoa katika mpira wetu, NMB, TBL na zaidi. Ukweli ni kwamba fedha inayowekezwa kwa sasa ni ndogo sana ikilinganishwa na thamani ya Simba iliyonayo hivi sasa.

 

Ni kweli kwamba kutokana na makubaliano ya kipindi hicho na ni sahihi kwa kipindi hicho SportPesa walikuwa wakombozi wa vilabu vyetu kwa sababu TBL walijiondoa hivyo walitusaidia, lakini uhalisia kwasasa kuna haja ya kutafakari upya.Mtu ambaye tunafanya naye kazi ndiye anapewa kipaumbele katika makubaliano ya mkataba mpya ili kuboresha.

 

 

”Iwapo hakutokuwa na maslahi, ni bora hata utoe nafasi bure kusaidia jamii kuliko kuendelea kutangaza na kupokea kiasi ambacho hakiendani uhalisia wa thamani ya klabu yetu,” amesema Mulamu Ng’ambi, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba.


KONDE BOY WA SIMBA CHAGUO LA GOMES ATAJA KINACHOMPA FURAHA MTAMBO WA MABAO AZAM FC WAREJEA KAZINI, KUIVAA MTIBWA SUGAR

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply