Simba SC

BASI LA SIMBA SC LAWEKWA SOKONI

admin April 3, 2021 9:47 am

 


MWAKA mpya na mambo mapya ndani ya kikosi cha Simba, mara baada ya kuliweka sokoni basi lao la timu ambalo wamekuwa wakilitumia kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Viongozi wa Simba wameyasema hayo baada ya kusambaa picha mitandaoni zikionyesha basi jipya likiwekwa stika zenye nembo za klabu hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barabara Gonzalez aliliambia Championi Jumamosi kuwa, wapo kwenye mpango wa kubadilisha basi hilo na kununua jipya, hivyo wameliweka sokoni basi lao la sasa ili wapate fedha ya kuongezea gharama za kununua basi jipya.

“Unajua hata ukitaka kununua simu mpya, lazima uuze ile ya zamani kwanza, kisha uongeze hela za kununua hiyo simu. Ndiyo tulichokifanya sisi tunataka kuliuza basi letu la zamani ili tununue jipya,” alisema Barbara

MEDDIE KAGERE: TUTAINGIA NA LENGO MOJA DHIDI YA AS VITA NYOTA SITA WASIMAMISHWA NDANI YAPOLISI TANZANIA, RASHID JUMA WA SIMBA NDANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply