Home Simba SC MAJINA MAWILI YA NYOTA WA SIMBA YAPENYA CAF

MAJINA MAWILI YA NYOTA WA SIMBA YAPENYA CAF


MAJINA ya nyota wawili wa Simba yametajwa kwenye kikosi bora cha Ligi ya Mabingwa Afrika katika raundi ya tano.

Mashindano haya makubwa kwa bara la Afrika ambayo yanasimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) yanafuatiliwa na watu wengi ambapo Simba imekuwa ikitajwa kuwa moja ya timu zinazofuatiliwa kwa ukaribu.

Sababu kubwa ya wawakilishi hawa wa Tanzania kufuatiliwa ni utofauti wao kwa msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuwa tofauti na misimu iliyopita.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kwa msimu wa 2020/21 imeweza kuwa imara katika mechi zake za kimataifa jambo ambalo limewafanya kuweza kutinga hatua ya robo fainali wakiwa ni vinara wa kundi A.

Pointi zao 13 kibindoni zimekuwa zikisakwa na wachezaji wake ambao amekuwa akiwafanyia mabadiliko kidogo na kwa raundi hii ni Luis Miquissone ambaye ni kiungo mshambuliaji pamoja na mshikaji wake Clatous Chama. 

SOMA NA HII  ACHANA NA NASHON....MUDATHIRI YAHAYA NAYE MBIONI KUTUA MSIMBAZI...DILI LIKO HIVI..