Home Simba SC CHAMA, LUIS WAFICHWA MISRI

CHAMA, LUIS WAFICHWA MISRI

 

WAKIWA wanajiandaa na mchezo wao wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya klabu ya Al Ahly, Uongozi wa klabu ya Simba umelazimika kuwaongeza ulinzi nyota wa kikosi chao hasa Luis Miquissone na Clatous Chama ambao wameonekana kusakwa tangu kikosi chao kilipotua.

Taarifa za kuaminika kutoka chanzo cha karibu cha Simba kimetutonya kuwa tangu walipotua kwenye uwanja wa ndege wa Cairo juzi Jumatano, wakazi wengi wa jiji la Cairo wamekuwa wakitafuta nafasi ya kuwaona wachezaji wa Simba huku Luis na Chama wakionekana kuuliziwa zaidi.

Nyota hao wawili wiki iliyopita walichaguliwa kuingia ndani ya kikosi bora cha Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuhusika katika mabao yote manne waliyoyapata katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya AS VIta, ambapo Chama pia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa wiki wa michuano hiyo.

SOMA NA HII  AMBANGILE:- HAWA WATOTO WA SIMBA WAVUMILIWE SANA...