Ligi Kuu

YANGA YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA KMC KWA MKAPA

admin April 10, 2021 6:47 pm

 


KIKOSI cha Yanga leo kimelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.


Ni David Bryson wa KMC alianza kupachika bao la kuongoza dk 28 kipindi cha Kwanza lilisawazishwa na Yacouba Sogne dk 46 kipindi cha pili. 

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba zama za Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo ulikamilika kwa ubao kusoma KMC 1-2 Yanga.

Ikiwa nyumbani KMC haikuwa na chaguo zaidi ya kuruhusu pointi tatu zake zikisepa mazima mbele ya Yanga ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara.

Mshambuliaji wa KMC, Charles Ilanfya atajilaumu mwenyewe kwa kuwa alikosa nafasi ya wazi kipindi cha Kwanza akiwa yeye na mlinda mlango Farouk Shikalo baada ya kupiga shuti ambalo lilikwenda nje kidogo ya lango.


BAADA YA MECHI , KOCHA AL AHLY AMTAJA AISHI MANULA VIDEO: KMC, HAIKUWA BAHATI YETU, ALIA NA FAULO ILIYOLETA BAO KWA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply