CAF

NAMUNGO YAPOTEZA MBELE YA NKANA ZAMBIA KOMBE LA SHIRIKISHO

admin April 12, 2021 5:47 am

 

NAMUNGO FC Wawakilishi  wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika,walipoteza kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia, ukiwa ni mchezo wa nne wa michuano hiyo hatua ya makundi ambapo timu hizo zipo Kundi D.


Dakika 90 zilikamilika kwa ubao kusoma Nkana FC 1-0 Namungo na kufanya ipoteza jumla ya mechi zote nne ambazo imecheza mpaka sasa na ipo nafasi ya nne bila pointi. 


Katika mchezo uliopita baina ya timu hizo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Namungo ilikubali kichapo cha bao 1-0.

 

Akizungumza na Saleh JembeMorocco amesema:”Ni uzoefu ambao unatupatia shida na kutufanya tusipate matokeo mazuri.


“Mapungufu ambayo tunayaona tutayafanyia kazi ili kupata matokeo kwenye mechi zetu zijazo,” .


Bao la ushindi kwa Nkana FC lilipachikwa na Fredy Tshemega dakika ya 71.


MANCHESTER UNITED YAPINDUA MEZA KIBABE MBELE YA TOTTENHAM YANGA: LIGI YA TANZANIA NI NGUMU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply