Azam FC

NADO AJIFUNGA MIAKA MIWILI AZAM FC

admin April 13, 2021 2:47 pm


Kiungo mshambuliaji wa AzamFC, Idd Seleman ‘Nado’, ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex.


Nado amesaini mkataba huo leo Jumanne Aprili 13 mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utakaomfanya aendelee kusalia Azam FC hadi mwaka 2024.


Nyota huyo amekuwa na kiwango tokea msimu uliopita alipojiunga Azam FC akitokea Mbeya City, hadi sasa msimu huu amehusika kwenye mabao 12 ya Azam FC, akifunga mara saba na kutoa pasi za mwisho tano.

STRAIKA AIPA SIMBA UBINGWA AFRIKA TANZIA: METACHA MNATA AFIWA NA MTOTO WAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply