Simba SC

DENSA: TUTAANZIA TULIPOISHIA

admin April 14, 2021 3:47 pm

 


BEKI wa kulia wa kikosi cha klabu ya Simba, Fatuma Issa ‘Fetty Densa’, amefunguka kuwa ana matumaini makubwa kikosi chao kitarejea na moto uleule wa kukusanya pointi tatu muhimu kwenye kila mchezo ili kutetea tena ubingwa wao msimu huu.

Simba Queens ndiyo vinara wa Ligi Kuu ya Wanawake ambapo mpaka sasa wamekusanya pointi 39 kwenye michezo 15 waliyocheza.

Akizungumzia, Densa amesema: “Kama mabingwa watetezi tumekuwa na mwendelezo mzuri msimu huu katika dhamira yetu ya kutetea ubingwa tulioutwaa msimu uliopita.

“Hivyo nina matumaini makubwa hata baada ya mapumziko haya ya dharura tuliyopata, kikosi chetu kitarudi na moto uleule wa kukusanya pointi tatu muhimu kwenye kila mchezo ulio mbele yetu,”

MANULA ATAJA SIRI YA KUWA BORA SIMBA YASHINDA 5G MBELE YA MTIBWA SUGAR KWA MKAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply