KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kimeeasili salama Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC, unaotarajiwa kuchezwa leo, Aprili 18 Uwanja wa Kambarage.
Mwadui FC inakumbuka kwamba mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma Simba 5-0 Mwadui FC ilikuwa ni zama za Sven Vandenbroeck ambaye kwa sasa amebwaga manyanga.
Pia Kocha Mkuu wa Mwadu FC alikuwa ni Khalid Adam ambaye naye pia alichimbishwa ndani ya Mwadui FC kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo.
Gomes amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho na wanaamini kwamba watapata matokeo chanya katika mchezo ambao utakuwa na ushindani.
“Tunahitaji kuona kwamba kwenye mechi zetu ambazo tutacheza tunapata matokeo mazuri kwani hakuna jambo lingine tunalohitaji kwa sasa zaidi ya pointi tatu,”.
Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya tatu imekusanya pointi 49 baada ya kucheza jumla ya mechi 21 kinara ni Yanga mwenye pointi 54 baada ya kucheza mechi 25.
Inakutana na Mwadui FC yenye pointi 16 baada ya kucheza mechi 25 msimu wa 2020/21 ikiwa nafasi ya 18.