Simba SC

MWANYI ZAHERA KUPEWA MAJUKUMU MATANO SIMBA

admin April 19, 2021 4:47 am


 IMEELEZWA kuwa aliyekuwa kocha wa zamani wa kikosi cha Yanga, Mwinyi Zahara yupo kwenye hesabu za mwisho kuajiriwa ndani ya Simba ili akamilishe majukumu matano kwa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu Didier Gomes.

Zahera baada ya kufukuzwa ndani ya Yanga aliweza kurejea tena Tanzania ambapo alikuwa ni Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi ndani ya Klabu ya Gwambina.

Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa majukumu ambayo yatakuwa mikononi mwa Zahera ni pamoja na:-

Uvumbuzi wa vipaji vya wachezaji ndani ya ardhi ya Tanzania. Kuwaendeleza wale wenye ujuzi ili waweze kuwa bora na imara.

Mshauri kwenye masuala ya usajili wa wachezaji ikiwa ni wale wa ndani ya Tanzania pamoja na wachezaji wa kigeni.

Kujishughulisha na masuala ya mikakati ya timu.

Kushughulikia masuala ya kibiashara pamoja na masoko.

MALENGO YA KMC MSIMU WA 2020/21 YAPO NAMNA HII SIMBA YAFANYA USAJILI MPYA LEO UPANDE MWINGINE KABISA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply