Azam FC

AZAM FC YAPANIA KULIPA KISASI MBELE YA YANGA KWA MKAPA

admin April 25, 2021 8:47 am


 KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amefunguka na 
kusema kuwa ingawa walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Yanga msimu huu katika Ligi Kuu Bara, mchezo wa marudio utakuwa upande wao katika kutaka kulipiza kisasi cha kufungwa.

Leo Jumapili, Aprili 25 Yanga na Azam FC zinatarajiwa kukipiga kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ukiwa mchezo wa Ligi Kuu Bara na timu zote zinawania kutwaa ubingwa.

Kocha Bahati amesema kuwa: “Ni kweli mchezo wa kwanza tulipokutana nao tulipoteza tukiwa nyumbani ila hiyo haitukatishi sisi tamaa ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu wa Jumapili.

”Kwa jinsi vijana wetu walivyo vizuri basi tuna imani ushindi tutaupata na tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo, mashabiki watupe sapoti.”

Azam inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 51 katika michezo 27, wakati Yanga ipo nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 57 katika michezo 26.

Mchezo unatarajiwa kuchezwa saa 2:15, usiku ule wa kwanza uliochezwa Azam Complex, ubao ulisoma Azam FC 0-1 Yanga.


MRITHI WA MIKOBA YA MGHANA NDANI YA YANGA ATOA NENO LA MATUMAINI SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU ISHU YA ZIMBWE  Jr KWENDA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply