kimataifa

BENZEMA AFIKISHA MABAO 71 UEFA, ZIDANE MATUMAINI KIBAO

admin April 28, 2021 10:47 am


 ZINEDINE Zidane, Kocha Mkuu wa Real Madrid amesema kuwa kwa kuwa bado wanaishi wana imani watakwenda kupata matokeo chanya kwenye nusu fainali ya pili dhidi ya Chelsea katika UEFA Champions League.

Nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Estadio Alfredo Di Stefano, ubao ulisoma Real Madrid 1-1 Chelsea jambo lililofanya asipatikane mbabe kwenye mchezo huo.

Ni Christian Pulisic dakika ya 14 alipachika mkwaju wa kwanza wa kuongoza uliwekwa usawa kibabe na nyota Karim Benzema dakika ya 29 na kumfanya afikishe jumla ya mabao 71 katika Uefa.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Chelsea, Thomas Tuchel amesema kuwa walishindwa kuumaliza mchezo huo kipindi cha kwanza ambacho walipata nafasi nyingi.

Zidane amesema hawakuwa na bahati ya kupata ushindi ila kwa kuwa bado wanaishi wana kazi ya kwenda kusaka ushindi kwenye mchezo wao watakapokwenda London.

“Bahati nzuri ni kwamba bado tunaishi na tuna kazi ya kwenda kutafuta ushindi London, hakuna mashaka tutajipanga ili kupata ushindi kwenye mchezo wetu ujao,” .

IHEANACHO AENDELEA KUWABEBA LEICESTER NIYONZIMA: NITAPAMBANA KURUDI KIKOSI CHA KWANZA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply