BAADA ya nahodha wa Tanzania Prisons, Benjamin Asukile kuweka wazi kuwa walizidiwa kwa kuwa refa hakuwa upande wao, Ofisa Habari wa Yanga amemtaka nahodha huyo aweze kuthibitisha suala hilo.
Jana, Uwanja wa Nelson Mandela kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, hatua ya 16 bora, ubao ulisoma Prisons 0-1 Yanga na kuwafanya Yanga watinge hatua ya robo fainali.
Asukile aliweka wazi kwamba walishindwa mchezo huo kwa kuwa mwamuzi hakuwa upande wao huku akisema kuwa bao ambalo walifungwa na Yacouba Songne lilikuwa halali.
Kupitia Ukurasa rasmi wa Istagram wa Hassan Bumbuli ameandika namna hii:-” Nahodha wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile ametoa tuhuma nzito dhidi ya Yanga, 1. Amesema tuliwazidi kwa sababu tulimuongeza Refa upande wetu, Hili tunataka alithibitishe, Kivipi na kwa namna gani!?
2. Walikuwa wakiwapigia simu na kutaka kutoa Mil 40 (Rushwa) Ili watuachie game, hili pia tunataka alithibishe mbele ya ya Mamlaka husika.
Hakuna namna ambayo Yanga tunaweza kuvumilia kuchafuliwa kwa kiwango hiki. Asukile anasahahu kwamba ushindi pekee ambao timu yake imewahi kuupata tangu msimu wa 2018/19 hadi sasa ni sare tatu tu katika mechi nane.
Msimu wa 2018/19 tuliwafunga mabao 3-1 kwao, pia tukawafunga 2-1 kwa Mkapa. Msimu wa 2019/20 tuliwafunga 1-0 kwao (Samora), wakaambulia sare kwa Mkapa na tukawatoa kwenye FA kwa mabao 2-0.
Msimu huu wamebahatika kupata sare mechi zote mbili za ligi, na jana wamekaa kwao, sasa huo ujasili wa Asukile na kujitoa ufahamu kuona wao ni wababe ameutoa wapi? Tutazifikisha tuhuma hizi zote kwa mamlaka husika ASAP.