KIPA wa kikosi cha Kagera Sugar, Chalamanda ambaye alikaa langoni wakati timu yake ikikubali kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora amesema kuwa alikuwa anapoteza muda ili kuwazuia wapinzani wao Simba wasiwafunge mabao mengi.
Ameweka wazi kwamba nyota wa Simba Bernard Morrison na Meddie Kagere ni wachezaji wazuri na Simba ni timu nzuri. Kutokana na tabia hiyo kwenye mchezo huo alionyeshwa kadi moja ya njano.